Ephesians 4

1Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita. 2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo. 3Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

4Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu. 5Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.

7Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo. 8Ni kama maandiko yasemavyo: “Alipopaa juu sana, aliongoza mateka katika utumwa. Akatoa vipawa kwa watu.”

9Ni nini maana ya, “Alipaa,” isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia? 10Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote.

11Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu. 12Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. 13Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.

14Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka. 15Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo. 16Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.

17Kwa hiyo, nasema hili, na nawasihi katika Bwana: Msitembee tena kama watu wa mataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao. 18Wametiwa giza katika mawazo yao. Wamefukuzwa kutoka katika uzima wa Mungu kwa ujinga ulio ndani yao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. 19Hawajisikii aibu. Wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu, katika kila aina ya uchoyo.

20Lakini, hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo. 21Nadhani kwamba mmesikia kuhusu yeye. Nadhani kwamba mmekuwa mkifundishwa katika yeye, kama tu ukweli ulivyo ndani ya Yesu. 22Lazima mvue mambo yote yanayoendana na mwenendo wenu wa zamani, utu wa zamani. Ni utu wa zamani unaooza kwa sababu ya tamaa za udanganyifu.

23Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu. 24Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.

25Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. “Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake,” kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake. 26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu. 27Msimpe Ibilisi nafasi.

28Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji. 29Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza. 30Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.

31Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi. Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

32

Copyright information for SwaULB